Posts

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA 1.    Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake msalabani Nilipewa uzima. Chorus: Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa.   2.    Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu, Uwezo na ushindi Hupatikana kwangu.”   3.    Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe.   4.    Sina wema moyoni, Nidai neema, Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa.   5.    Hata huko Mbinguni Miguuni pake, “Yesu alinifia,” Nitaimba milele.

88. NDIYO DAMU YA BARAKA

NDIYO DAMU YA BARAKA 1.    Ndiyo damu ya baraka ituoshayo wakosa, Kwake Bwana twaokoka, nasi twamsifu sasa; Nimestahili hukumu, siwezi kujitakasa; Nioshe katika damu, takuwa safi kabisa. Chorus: Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe katika damu; Takuwa safi kabisa.   2.    Yesu alivikwa miiba, na kuangikwa Mtini, Na maumivu si haba yaliyompata chini. Nataka kijito hicho niende kuoga sasa; Ndicho kinitakasacho, nami ni safi kabisa.   Chorus: Safi kabisa; safi kabisa! Ndicho kinitakasacho, Nami ni safi kabisa.   3.    Baba, kweli nimekosa, moyo wangu ni dhaifu; Dhambi ni nyingi kabisa, nipate wapi wokovu? Yesu kijitoni pako, naja naamini sasa; Nioshe kwa damu yako, takuwa safi kabisa. Chorus:   Safi kabisa; safi kabisa! Nioshe kwa damu yako, Nami ni safi kabisa.

89. KWA KALVARI

KWA KALVARI 1.    Muda mwingi nilipotea, Sikufahamu msalaba, Wala aliyenifilia, Kwa Kalvari.   Chorus: Rehema bure na neema, Samaha nalo nilipewa, Ndipo aliponifungua, Kwa Kalvari.   2.    Kwa neno lake Bwana Mungu, Nilijiona mimi mwovu, Nikageuka na kutubu, Kwa Kalvari.   3.    Yote kwa Yesu namtolea, Ndiye mfalme wa pekee sasa, Kwa furaha nitamwimbia, Kwa Kalvari.   4.    Jinsi pendo lilivyo kuu, Neema ilishuswa toka juu, Alitufanyia wokovu, Kwa Kalvari.

90. ALITESWA, ALITESWA

ALITESWA, ALITESWA 1.    Aliteswa, aliteswa, Msalabani Yesu aliteswa, Dhambi zangu ameziondoa, Mahali pangu aliumizwa.   2.    Alikufa, alikufa, Msalabani Yesu alikufa, Kwa kifo chake nakombolewa, Kwa kuwa Yesu alinifia.   3.    Kafufuka, kafufuka, Kaburini Yesu alitoka, Nami nimewekwa huru pia, Kwa kuwa Yesu alifufuka.   4.    Yuko hai, yuko hai, Mbinguni anaishi Mwombezi, Daima huniombea mimi, Kwa kuwa Yesu adumu hai.   5.    Atarudi, atarudi, Siku moja Yesu atarudi, Na tutamwonapo tutafurahi, Kwa kupelekwa kwake Mbinguni.   6.    Sifa kwake, sifa kwake, Mbinguni na huimbwa milele, Kwa furaha, masifu, na shangwe, Tutamwimbia Yesu milele.

91. MAPENZI YAKO YAFANYIKE BWANA

MAPENZI YAKO YAFANYIKE BWANA 1.    Mapenzi yako yafanyike, Wewe mfinyanzi, nami towe, Unifinyange upendavyo, Mimi tayari, naja kwako.   2.    Mapenzi yako yafanyike, Unihojie dhambi zote, Unisafishe vya kimwili, Niinamapo Msalabani.   3.    Mapenzi yako yafanyike, Mimi dhaifu, mimi mnyonge. Uwezo wote, kwako kweli, Sasa niponye, Ee, Mwokozi.   4.    Mapenzi yako yafanyike, Natoa kwako vitu vyote, Maisha, mali, moyo, mwili, Vyote ni vyako, kweli, kweli.   5.    Mapenzi yako yafanyike, Mapenzi yangu yavunjike, Ninakubali uwe Bwana, Ni mali yako, twaa kabisa.   6.    Mapenzi yako yafanyike, Unitawale siku zote, Sura ya Yesu umba kwangu, Nijaze Roho nayo nguvu.

92. NATAKA NIMJUE YESU

NATAKA NIMJUE YESU 1.    Nataka nimjue Yesu, Na nizidi kumfahamu, Nijue pendo lake, na Wokovu wake kamili.   Chorus: Zaidi, zaidi, nimfahamu Yesu, Nijue pendo lake, na wokovu wake kamili.   2.    Nataka nione Yesu, Na nizidi kusikia, Anenapo kitabuni, Kujidhihirisha kwangu.   3.    Nataka nifahamu, na Nizidi kupambanua Mapenzi yake, nifanye Yale yanayompendeza.   4.    Nataka nikae naye, Kwa mazungumzo zaidi, Nizidi kuwaonyesha Wengine wokovu wake.

93. BWANA AMEFUFUKA

BWANA AMEFUFUKA 1.    Bwana amefufuka, Aleluya. Twimbe na malaika, Aleluya. Sifa zetu na shangwe, Aleluya. Na zao zisitengwe, Aleluya.   2.    Ukombozi timamu, Aleluya. Umetimu kwa damu, Aleluya. Mshindi asifiwe, Aleluya. Yu hai kwa milele. Aleluya.   3.    Jiwe, lindo, muhuri, Aleluya. Vi wapi? Na kaburi? Aleluya. Kifo hakimuweki, Aleluya. Ametoka peponi, Aleluya.   4.    Yu hai mtukufu; Aleluya. Cha kifo hatuhofu! Aleluya. Alitufia sisi, Aleluya. Tuwe mahuru nasi, Aleluya.   5.    Kichwa chatangulia, Aleluya. Tupae, nasi, pia!, Aleluya. Kwa kuwa tuna fungu, Aleluya. Mti, kaburi, mbinguni, Aleluya.   6.    diwe Mwokozi wetu, Aleluya. Sifa ni yako Yesu, Aleluya. Utukuzwe pekeo, Aleluya. Ni wewe ufufuo, Aleluya.