87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA
DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA 1. Deni yangu ya dhambi, Yesu amelipa. Kwake msalabani Nilipewa uzima. Chorus: Deni ya dhambi, Msalabani, Ilimalizikia, Ni huru kabisa. 2. Bwana Yesu asema, “Mwanangu dhaifu, Uwezo na ushindi Hupatikana kwangu.” 3. Bwana, kweli naona, Nguvu zako pekee Huondoa ukoma, Niwe kipya kiumbe. 4. Sina wema moyoni, Nidai neema, Nakubali kabisa, Kwa damu kusafiwa. 5. Hata huko Mbinguni Miguuni pake, “Yesu alinifia,” Nitaimba milele.