106. MUNGU AWE NANYI DAIMA

MUNGU AWE NANYI DAIMA

1.  Mungu awe nanyi daima,
Hata twonane ya pili,
Awachunge kwa fadhili,
Mungu awe nanyi daima.

Chorus:
Hata twonane huko juu,
Hata twonane kwake kwema;
Hata twonane huko juu,
Mungu awe nanyi daima.
 
2.  Mungu awe nanyi daima;
Ziwafunike mbawaze,
Awalishe, awakuze;
Mungu awe nanyi daima.
 
3.  Mungu awe nanyi daima;
Kila wakati wa shani
Awalinde hifadhini;
Mungu awe nanyi daima.
 
4.  Mungu awe nanyi daima;
Awabarikie sana,
Awapasulie kina;
Mungu awe nanyi daima.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA