102. KAZI YANGU IKIISHA

KAZI YANGU IKIISHA
 
1.  Kazi yangu ikiisha, nami nikiokoka;
Na kuvaa kutokuharibika,
Nitamjua Mwokozi nifikapo ng’amboni;
Atakuwa wa kwanza kunilaki.
 
Chorus:
Nitamjua, nitamjua, nikimwona uso kwa uso;
Nitamjua, nitamjua, kwa alama za misumari.
 
2.  Furaha nitapata nikiona makao
Bwana aliyotuandalia;
Nitamsifu mwokozi kwa rehema na pendo
Vilivyonipa pahali Mbinguni.
 
3.  Nao waliokufa katika Bwana Yesu,
Nitawaona tena huko juu;
Lakini nifikapo kwake huko Mbinguni,
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.
 
4.  Milangoni mwa mji Bwana atanipisha,
Pasipo machozi wala huzuni.
Nitauimba wimbo wa milele; lakini
Nataka kumwona Mwokozi kwanza.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA