111. NENO LAKO BWANA

NENO LAKO BWANA
 
1.  Neno lako, Bwana,
Ni imara sana;
Lilo latwongoza,
Lilo latufunza.
 
2.  Adui wabaya
Wakikaribia,
Neno lake Bwana
Ni ulinzi sana.
 
3.  Siku za dhoruba
Soma ukiomba;
Neno lake Bwana
Msaada sana.
 
4.  Ukiliamini,
Hwenda na amani;
Una na furaha
Neno ni silaha.
 
5.  Ni furaha kweli,
Na wingi wa mali,
Neno lake Bwana
Kwa wasiokana.
 
6.  Neno la rehema,
Tukali wazima;
Faraja I papo,
Tufarikanapo.
 
7.  Tulijue sana,
Neno lako, Bwana,
Hapa tukupende,
Kisha kwako twende.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA