103. KAA NAMI

KAA NAMI

1.  Kaa nami, ni usiku tena;
Usiniache gizani, Bwana;
Msaada wako haukomi;
Nili peke yangu, kaa nami.
 
2.  Siku zetu hazikawi kwisha,
Sioni la kunifurahisha;
Hakuna ambacho hakikomi,
Usiye na mwisho kaa nami.
 
3.  Nina haja nawe kila saa;
Sina mwingine wa kunifaa;
Mimi nitaongozwa na nani
Ila wewe Bwana, kaa nami.
 
4.  Sichi neno uwapo karibu;
Nipatalo lote, si taabu;
Kifo na kaburi haviumi;
Nitashinda kwako, kaa nami.
 
5.  Nilalapo nikuone wewe,
Gizani mote nimulikie;
Nuru za mbinguni hazikomi,
Siku zangu zote kaa nami.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA