107. EWE, BABA WA MBINGUNI

EWE, BABA WA MBINGUNI
 
1.  Ewe, Baba wa Mbinguni,
Usikie twombalo
Hapa chini duniani,
Na uwe radhi nalo.
 
Chorus:
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
Ee Mungu, bariki
Ndugu hawa wawili!
 
2.  Watu hawa mbele zako,
Na mbele ya kanisa;
Watimize Neno lako
Wanakutana sasa.
 
3.  Kama Yesu na Kanisa,
Ni mmoja, na hivyo,
Watu hawa wape sasa
Wawe mmoja vivyo.
 
4.  Walinde, Bwana, daima,
Wabariki nyumbani
Uwape nyingi salama
Humu ulimwenguni.
 
5.  Wabariki, ewe Bwana,
Watu hawa wawili,
Wape upaji wa wana,
Wafurahishwe kweli.
 
6.  Siku zao duniani
Zitakapopungua,
Wape kurithi Mbinguni
Mema ya kwendelea.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA