98. HUYO NDIYE! ANASHUKA

HUYO NDIYE! ANASHUKA

1.  Huyo ndiye! anashuka,
Aliyetufilia,
Wengi waliookoka,
Wakimfurahia,
Aleluya!
Yesu aturudia.
 
2.  Sote tutamtazama,
Amekaa kitini,
Nao waliomchoma,
Kumkaza mtini,
Na kilio, wamuone enzini.
 
3.  Alama za kifo chake
Hata sasa anazo
Na waaminifu wake
Wapendezewa nazo.
Alipata,
Kwetu alama hizo.
 
4.  Wokovu utakiwao
Sasa wapatikana,
Na watakatifu hao
Mbinguni wakutana
Kumlaki,
Ndiyo siku ya Bwana
 
5.  Wakusujudie wote
Mbele ya kiti chako.
Zako, Bwana, nguvu zote
Itwae miliki yako
Njoo Bwana,
Sisi tu watu wako.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA