108. TWENENDE SAYUNI

TWENENDE SAYUNI

1.  Mpendao Bwana
Ije raha yenu!
Imbeni nyimbo za raha
Wa ibada yenu.

Chorus: 
Twenende Sayuni,
Mji mzuri Sayuni;
Twenende juu Sayuni
Ni maskani ya Mungu.
 
2.  Wasiimbe wao
Wasioamini,
Watoto wa Mungu ndio
Waimbao chini.
 
3.  Twaona rohoni
Baraka za Mungu,
Tusijafika Mbinguni
Kwenye utukufu.
 
4.  Tutakapo mwona
Masumbuko basi,
Huwa maji ya uzima,
Anasa halisi.
 
5.  Tupaaze sauti,
Na fute machozi,
Twenenda kwa Imanweli
Naye ni Mwokozi.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA