104. TWASOMA NI NJEMA SANA

TWASOMA NI NJEMA SANA

1.  Twasoma, ni njema sana
Mbinguni, kwa Bwana;
Twasoma, dhambi hapana,
Mbinguni kwa Bwana;
Malaika wema wako,
Vinanda vizuri viko,
Na majumba tele yako,
Mbinguni kwa Bwana.
 
2.  Siku zote ni mchana,
Ni nchi ya raha;
Wala machozi hapana,
Ni nchi ya raha;
Walioko wauona
Uso wa Mwokozi, tena
Jua jingine hapana,
Ni nchi ya raha.
 
3.  Nyama na vitu viovu
Havimo kabisa;
Kifo nacho, na ubovu,
Havimo kabisa.
Ni watakatifu wote,
Wameoshwa dhambi zote;
Wasiosafiwa wote
Hawamo kabisa.
 
4.  Tuna dhambi, pia sote,
Mwokozi akafa;
Kwake tutaoshwa zote,
Mwokozi akafa;
Kwake twapata wokovu,
Tutawona utukufu;
Mbinguni tutamsifu;
Mwokozi akafa.
 
5.  Baba, mama, ndugu zetu,
Twendeni kwa Bwana;
Huku chini sio kwetu,
Twendeni kwa Bwana;
Tusishikwe na dunia,
Na dhambi kutulemea;
Tutupe vya chini pia,
Twendeni kwa Bwana.

Comments

Popular posts from this blog

87. DENI YA DHAMBI ILIMALIZIKA

110. MAPYA NI MAPENZI HAYO

88. NDIYO DAMU YA BARAKA